Jokate Mwegelo ambaye hivi karibuni alishoot video ya wimbo wake wa kwanza kama msanii wa muziki nchini, ametoa sababu za kwanini mpaka sasa video wala wimbo huo havijafanikiwa kutoka.
Jokate a.k.a Kidoti amesema kuwa video aliyoshoot Kenya imechelewa kwasababu kuna vitu ambavyo hakuvipenda katika video, hivyo vimechukua muda kurekebishwa ili kupata kitu bora zaidi.“Kuna delay zilitokea kwenye utayarishaji kidogo,sikupenda end product.
Cause napenda niwape fans the besssssssst. So nawaomba wanivumilie kidogo. Ndio maana sipo kwenye social networks now, napiga kazi zaidi nisicheleweshe zaidi.”