Taswira kutoka katika eneo la ajali hiyo.
WATU 12 wamefariki huku 45 wakijeruhiwa baada ya treni mbili za abiria kugongana usiku wa kuamkia leo katika Jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
Ajali hiyo iliyohusisha treni ya Krishak Express, iliyokuwa ikisafiri kutoka Varanasi kwenda Gorakhpur iliyogongana na treni ya Barauni Express ilitokea karibu na Kituo cha Gorakhpur kilichopo kilomita 270 (maili 167) kutoka Makao Makuu ya jimbo hilo, Lucknow.