Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKURANGA -PWANI)
Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa kata ya Kimanzichana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo leo
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo.
Baadhi ya wananchi wakipunga mikono kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kimanzichana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano mjini Kimanzichana, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali pamoja na wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth Development ambapo amekipa kikundi hicho mashine 2 ili kuongeza uwezo wa kikundi hicho. Mmoja wa wanakikundi wa kikundi cha Mkuranga Youth Development Bi Faraja Msani akionyesha jinsi wanavhoshiriki shughuli za kujiletea maendeleo. Wananchi wakishiriki kukusanya matofali katika shule ya sekondari ya Mwarusembe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli ya ujenzi wa mafarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe huku wananchi wakiendelea na kazi ya kukusanya matofali. Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mwarusembe.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kutoka Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi
Mmoja wa viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Bi Agricola akiwa katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment